GET /api/v0.1/hansard/entries/352249/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 352249,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/352249/?format=api",
    "text_counter": 209,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mung’aro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 76,
        "legal_name": "Gideon Mung'aro Maitha",
        "slug": "gideon-maitha"
    },
    "content": "Asante sana mhe. Spika. Nataka pia nichukue nafasi hii nikupongeze kwa kuchaguliwa kama Spika wa Bunge hili. Vile vile, ningependa kuchukua nafasi hii kuwashukuru watu wa Kilifi Kaskazini kwa kunipatia nafasi kuwa mbunge wao wa kwanza katika eneo hilo jipya la Bunge. Mhe. Spika, katika kuchangia Hotuba ya Rais, ningependa kutilia mkazo jambo ambalo ndugu yangu Aburi amelizungumzia; hasa upeanaji wa tarakirishi kwa watoto wa darasa la kwanza katika shule zetu za msingi. Nafikiri ijapokuwa Rais ana maono mema katika kuanzisha mradi huu wa tarakirishi kwa watoto wetu wa darasa la kwanza, ingekuwa vyema ikiwa Rais, badala ya kuwapatia wanafunzi wa darasa la kwanza tarakirishi hizo ambazo zinaweza kuhatarisha usalama wa watoto wetu wadogo badaye--- Kwa sababu watu watajaribu kuwapokonya. Hata zinaweza kuibiwa zikiwa nyumbani. Watu wanafikiria ni vifaa ambavyo vinaweza kuwasaidia kwa njia nyingi. Serikali ingejenga mahabara katika shule zetu zote za msingi ile watoto wetu wa kutoka darasa la kwanza hadi la nane waweze kufaidika kutokana na mradi huu wa tarakirishi. Vile vile, mhe. Spika ningetaka kuzungumzia kuhusu Hotuba ya Rais, hasa kuhusu swala la ardhi. Sisi watu wa Pwani, swala la ardhi ni swala nyeti sana. Watu wa Pwani wamekuwa maskwota tangu wakati wa uhuru wa nchi hii. Swala la ardhi katika"
}