GET /api/v0.1/hansard/entries/352252/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 352252,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/352252/?format=api",
"text_counter": 212,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Pwani limetumiwa wakati wa kampeini za kutafuta kura za urais na hata za ubunge. Swala la ardhi limeleta uhasama katika Pwani. Limeleta vuguvugu la Mombasa Republican Council (MRC). Tunasema Serikali hii isitumie ardhi kama chombo cha kampeini au kuwaweka Wapwani pamoja. Lakini Serikali itatue swala hili, ili, ifikapo mwaka wa 2017, liziwe swala la kampeini tena ama kuomba kura. Bali, tatizo la ardhi liwe limemalizwa katika Mkoa wa Pwani. Swala lingine muhimu katika Mkoa wa Pwani, ambalo limeleta matatizo mengi na vijana kuanza kujiunga na vikundi, ni swala ambalo Rais alizungumzia katika Hotuba yake. Ni swala la ufufuaji wa viwanda. Kuna wengi waliokuwa katika vikundi vya kijamii. Kule Pwani tulikuwa na viwanda kama kiwanda cha korosho katika Kilifi, kiwanda cha maziwa cha Mariakani na kiwanda cha Bixa kule Kwale. Ni viwanda ambavyo vikifufuliwa, vitatoa ajira kwa vijana wetu na kuweza kupunguza matatizo ya usalama katika eneo la Pwani. Swala lingine ambalo ni muhimu sana ni la unyunyisaji maji katika mashamba. Ni jambo ambalo Rais alilitilia mkaso sana. Ningependa kusema kwamba, kabla ya kuanza kunyunyisia maji mashamba, Rais na Serikali yake wahakikishe ya kwamba akina mama wetu wanaweza kupata maji karibu na kwa urahisi. Bado leo kuna akina mama wanaotembea zaidi ya kilomita ishirini ili kuchota maji ya matumizi. Vile vile, ningependa kuunga mkono swala la fedha kwa vijana wetu na akina mama bila riba. Lakini pesa hizo, hata kama zitagawanywa katika maeno ya uwakirishi Bungeni, ziwe rahisi kuwafikia vijana na akina mama wakati wanatafuta mkopo huo. Kwa sababu - kama nilivyosema hapo awali - wananchi wengi katika sehemu hii ni maskwota. Na kama kutatakikana vibali vya kuwaweza kupata pesa hizo za mkopo, basi itabidi---"
}