GET /api/v0.1/hansard/entries/352272/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 352272,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/352272/?format=api",
"text_counter": 232,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "nyingi kama yeye. Kwa hivyo, alipokuwa akizunguka kila mahali, alijua umuhimu wa watoto wa shule kuwa na laptop. Ningependa kusema kwamba mjukuu wangu mwenye umri wa miaka minne na nusu anajua kutumia simu ya rununu. Kwa hivyo, ni bora kuanza kuwafundisha watoto wetu kutumia komputa. Itakuwa jambo la kawaida kwao kutumia komputa wanapokua. Niliwasikia baadhi ya Wabunge wenzangu wakilalamika kuhusu stima. Si lazima uwe na stima ndiyo utumie laptop. Kuna stima kutoka kwa miale ya jua, ambayo inaweza kufanya kazi mpaka chini ya miti na hata chini ya kitanda. Kwa hivyo, kuanza kuwafundisha watoto wetu kutumia computa ni jambo la maana sana. Kuhusu suala la kuwaondolea akina mama kodi ya kujifungua hospitalini, ninamshukuru sana Rais lakini kuna jambo ambalo ningependa kuongezea. Tangu nilipochaguliwa, nimekuwa na shida ya maskini ambao wamekuwa na shida ya kutoa miili ya watoto wao kutoka kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti. Tukiwauliza Wabunge walioko hapa watathibitisha kwamba shida kubwa inayotukabili ni malipo ya gharama za kuhifadhi maiti. Kuna haja ya kuliangazia jambo hili. Nilikuwa na mtu mmoja mwenye shida hiyo juzi. Nikawa na mwingine leo. Nilipoenda hospitali niliambiwa ni lazima nilipe pesa kidogo halafu nionyeshe kwamba tuna njia ya kuweza kutafuta pesa hizo, kama vile Harambee ama njia nyingine yoyote. Kama tunavyojua, Harambee imesimamishwa. Kwa hivyo, ninaomba suala la malipo ya kuhifadhiwa maiti liangaziwe ili maskini wapewe nafasi ya kupumua. Kuhusu kilimo, Rais alizungumza mambo mazuri sana lakini kuna jambo ambalo limetokea. Katika sekta ya ukulima, tungepitisha sheria kwamba si lazima mbolea iuzwe kwa kilo hamsini. Ukiangalia wale maskini ambao wana shamba ndogo, utakuta kwamba hawawezi kutumia mbolea kwa sababu hawana pesa ya kuinunua. Ningependa jambo hili liangaziwe sana. Mbolea inafaa ipimwe kwa kiwango ambacho maskini anaweza kununua. Mbolea inafaa ipimwe katika kilo kumi au kilo 20 ili maskini aweze kuitumia ili apate mazao ya kutosha. Inafaa tuzingatie mambo haya wakati tunapojadiliana hapa. Kuna mambo ambayo tunaongea lakini hayaonyeshi mapenzi yetu kwa wenye kutuchagua."
}