GET /api/v0.1/hansard/entries/352334/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 352334,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/352334/?format=api",
"text_counter": 294,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Lay",
"speaker_title": "Taita Taveta County Women Representative",
"speaker": {
"id": 1022,
"legal_name": "Joyce Wanjalah Lay",
"slug": "joyce-wanjalah-lay"
},
"content": " Ahsante sana mhe. Spika. Ningependa kukupongeza kwa kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge hili. Aidha ningependa kuwapa shukrani kubwa wakaazi wa Taita Taveta kwa kunichagua kama mwakilishi wao. Natoa shukrani kubwa kwa Rais. Kuna mambo machache katika hotuba yake ambayo ningependa kuangazia ambayo aliyataja kwa uzito sana. Kwanza ni elimu. Yeye anataka kupeleka elimu yetu katika kiwango cha juu. Alitaja mambo ya laptops. Sisi tuliochaguliwa kama viongozi inatupasa tuangazie masuala ya elimu ikiwa tutataka kupeleke elimu katika ngazi ya juu. Tukiseme tutawapatia watoto laptop na walimu waendelee kugoma kwa ajili ya mambo ya mishahara basi elimu haitakuwa imepanda katika kiwango cha juu. Rais aliangazia suala la mashamba. Suala la ardhi ni nyeti katika nchi yetu yote. Mimi nikiwa mkazi wa pwani naweza kusema kwamba suala hili lilimnyima Rais kura kule pwani. Ukweli lazima tuusema. Hata kama tungeenda raundi ya pili bado tusingempa kura kwa ajili ya jambo hilo. Ni jambo ambalo limeleta utata sana pale pwani. Wakazi wa pwani wengi hawajamiliki ardhi. Hawana vyeti vya ardhi. Hii imeleta machungu kwa miaka mingi. Naiomba serikali hii pamoja na viongozi waliochaguliwa waweze kutatua suala hili ili lisitumiwe wakati watu wanatafuta kura, kwa mfano, kuzawadia watu ekari fulani za ardhi. Kitu ambacho unapeana wakati unatafuta kura hatutahesabu. Ni kama vile unaenda kuchumbia msichana mrembo. Unapomchumbia unampa zawadi hapa na pale. Wakati unapomwoa hutohesabu kwamba ulimpa hiki ama kile. Wakati umemwoa ni jukumu lako kumtunza. Kwa sababu Rais Uhuru amepata nafasi ya kuongoza nchi hii, ninayo matumaini kwamba ataliangazia suala hili la ardhi ili liwe ni historia. Amalize mambo haya wakati huu akiwa kiongozi. Masuala yote ambayo watu wa Mkoa wa Pwani wanataka kumwuliza sasa wanayo fursa kufanya hivyo. Mhe. Spika, vile vile, Rais alizungumzia utalii. Katika Kaunti ya Taita Taveta tuna shida ya ugomvi baina ya wanyamapori na binadamu. Haswa, upande wa Mwakitao, kila wakati unapata kwamba binadamu wameuawa na mimea kuharibiwa na wanyama. Ninajua kwamba tunaweza kupata suluhu ya hali hii. Wakenya wako na matumaini mengi sana kwa sababu ya huu uongozi ambao umekuja katika mfumo wa katiba mpya. Ni matumaini ya Wakenya kwamba tutaweza kuitekeleza Katiba na kuangazia masuala yanayowadhuru, ugomvi baina ya wanyamapori na binadamu likiwa mojawapo. Nimepata fursa ya kuwasikiza viongozi kutoka matabaka mbalimbali. Suala lililoibuka ni kwamba shida ya maji imeenea katika taifa nchi yetu ya Kenya. Sitasema kwamba shida hiyo iko Taita Taveta peke yake ama kwenye eneo la pwani peke yake. Kila mmoja wetu hapa ameangazia masuala ya maji na barabara. Kwa hivyo, tukishirikiana kama viongozi, tunaweza kuzitatua shida hizi, kwa sababu ukimpatia binadamu maji ni kama kwamba umempatia dawa."
}