GET /api/v0.1/hansard/entries/354350/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 354350,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/354350/?format=api",
"text_counter": 211,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Shukrani Mhe.Naibu Spika kwa kuniokoa. Naomba kuchangia Hotuba ya Rais kama alivyotupatia wakati wa kufungua Bunge letu. Naipongeza sana hotuba ya Rais wetu kwa sababu iliguzia mambo muhimu; hususan yale yalionileta katika Bunge hili. Kwanza, ni kuhusu ada zinazolipiwa na kina mama wakati wa kujifungua. Nashukuru kwamba jambo hilo limeweza kutatuliwa. Na pia ametupatia nafasi hususan sisi watu wa Pwani tuweze kuzaana kwa wingi kwa sababu inaonekana mkiwa wengi ndio mnaweza kupata urais katika hii nchi. Pia itaweza kutusaidia kwa sababu hali ya umaskini imekidhiri sana katika Jimbo letu la Kwale na Pwani kwa ujumla. Kwa upande wa elimu, Rais alisema kwamba tarakirishi zitapatikana kwanzia mwaka ujao. Swali langu ni je, nani atawafunza watoto hao kutumia tarakirishi-beba? Hata walimu wenyewe hawatoshi katika shule. Hata hawana elimu ya kutumia tarakirishi-beba. Kwa hivyo, nilikuwa natarajia kwamba Rais atatupatia ratiba ya kuajiri walimu zaidi katika shule na waanze kupewa elimu kabla ya mwaka ujao. Tukiangazia usalama, hatuzungumzii tu kuwa na askari wengi. Nilikuwa natarajia Rais wetu atatueleza vile ataweza kutatua yale madhambi yaliyotendewa watu wa Pwani. Madhambi yaliyotendewa watu wa Pwani ndio chanzo cha kutokuwa na usalama katika eneo letu la Pwani. Tunadai mambo yetu ya ardhi na ajira. Kwa mfano, ukiingia katika Wizara ya Fedha, kuanzia âAâ hadi âZâ ni watu wa kabila moja! Rais hakutueleza vile atatatua mambo kama hayo. Tunataka usawa; sio usawa wa jinsia bali usawa katika ugavi wa mamlaka katika kila eneo, ili tuweze kuwa na usalama katika nchi hii yetu ya Kenya. Jambo lingine ni kuhusu mambo ya kilimo. Rais alisema kwamba ataweza kuboresha ukulima. Ukulima hauwezi kuboreshwa ikiwa kwanza wenyeji wa zile sehemu zenye utata wa ardhi hawana hata zile sitakabadhi za kumiliki ardhi hizo. Kwa hivyo, kwanza, Rais atuwezeshe kupata mashamba yetu ndio tuweze kuzungumzia jinsi kilimo kitaboreshwa katika Pwani. Nikimalizia, natambua juhudi za Rais kuwasaidia akina mama na vijana ili waweze kujimudu kimaisha. Zile pesa ambazo zimetengwa zije kwetu, nilikuwa natarajia Rais, ijapokuwa anasema zitelemshwe ziende kwa maeneo ya Bunge, lakini angetaja ni nani atakuwa msimamizi. Ningeomba pesa hizo zielekezwe katika majimbo ziweze kuwa katika mikono ya akina mama waakilishi wa majiimbo. Kwa sababu, sisi akina mama tumeletwa katika Bunge hili lakini hatukuelezwa tutakuwa tunatumia vyombo gani katika kuendesha mipangalio ya"
}