GET /api/v0.1/hansard/entries/354372/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 354372,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/354372/?format=api",
    "text_counter": 233,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
    "speaker_title": "The Member for Lamu East",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Asante Naibu Spika. Ninaitwa Shariff Athman Ali. Ningependa kuchukua fursa hii kukupongeza wewe pamoja na Spika kwa kuchaguliwa katika nafasi zenu. Vile vile, ninataka kuchukua fursa hii kuwashukuru watu wa Lamu Mashariki kwa kunichagua kuwawakilisha katika Bunge hili la kumi na moja. Kulingana na Hotuba ya Rais iliyotolewa hapa wiki iliyopita, kwa kweli, ni Hotuba ya kupendeza. Kama unavyosikia Wabunge wenzangu--- Kila anayeinuka anaipendekeza Hotuba hii. Lakini ajabu kubwa iliyoko ni kwamba mpaka dakika hii yote yaliyozungumziwa--- Bali na kwamba Rais mstaafu Mwai Kibaki alianzisha CDF bado malalamiko mashinani yako. Vijana wanasoma chini ya miti. Hayo ni masikitiko makubwa na hatujui tuwalaumu viongozi waliotangulia au tuilaumu Serikali. Nikizungumzia maswala ya Lamu, leo hii akina mama kote nchini wanasherehekea wanasherehekea kwa sababu kutakuwa na huduma za uzazi za bure, lakini utashangaa kwamba katika Lamu Mashariki, hakuna hospitali za uzazi, na akina mama hawajui wajifungulie wapi. Kwa kweli, haya ni matatizo. Ni lazima tufahamu tunazungumzia nini na lipi litasuluhishwa."
}