GET /api/v0.1/hansard/entries/354373/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 354373,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/354373/?format=api",
"text_counter": 234,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
"speaker_title": "The Member for Lamu East",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Ukiangalia maswala ya ardhi, mpaka hivi sasa hili ni tatizo kubwa, na limezungumziwa na wapwani wenzangu. Swala hili linaihusu Lamu pia. Ningependa jambo hili lichukuliwe kwa uzito sana ili tusionekana kama ni nyimbo twaimba, ama ni hadithi tunatoa. Ni lazima tuonyeshe uzito wa maswala haya. Ni masikitiko na aibu kubwa katika nchi hii kuwa baada ya miaka 50 ya Uhuru, ama utawala wetu, bado kuna Wakenya ambao hawana maji, na kuna vijana ambao wanasomea chini ya miti kwa sababu hawana madarasa. Haya ni maswala ambayo ni lazima tuyape kipaumbele na kuyazingatia vilivyo. Kinachostahili hapa ni kuhakisha kwamba haya mambo yametekelezwa kikamilifu. Kuhusiana na usalama, juzi Lamu iliingiliwa na watu kutoka nchi jirani; waliingia kwa mahoteli, wakawachukua wazungu na wakaenda zao. Hali hii ilidhooofisha pakubwa utalii"
}