GET /api/v0.1/hansard/entries/354523/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 354523,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/354523/?format=api",
"text_counter": 384,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Dukicha",
"speaker_title": "The Member for Galole",
"speaker": {
"id": 1480,
"legal_name": "Hassan Abdi Dukicha",
"slug": "hassan-abdi-dukicha"
},
"content": " Asante sana, mhe. Naibu Spika. Kwa majina ninaitwa Hassan Dukicha, Mbunge wa eneo la uwakilishi Bungeni la Galole, Tana River. Shukrani zangu za kwanza zinaenda kwa watu wa Galole ambao walinichagua niwaakilishe katika Bunge hili. Ninawaambia asante. La pili nikukupongeza mhe. Naibu Spika kwa kuchaguliwa . Nilikuwa nakuunga mkono sana lakini niliona kama hukuwa unaniona, lakini sasa umeniona kidogo. Asante pia. Langu ni kuhusu hospitali ya Hola, katika sehemu ya Galole, ambayo ni eneo ninalowakilisha katika Bunge hili. Hospitali imegeuka kuwa nyumba ya panya, popo, na kila kitu. Haina vyombo vya kupima, kama mtambo wa picha, hakuna madaktari, dawa na pahali pa kuhifadhi maiti. Chumba cha kuhifadhi maiti hakipo kwa sababu ukiweka mwili wa binadamu, panya wanaula. Rais alitoa hotuba nzuri na ninataka kitu cha kwanza aangazie hospitali ya Hola kwa sababu iko katika hali mbaya."
}