GET /api/v0.1/hansard/entries/355328/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 355328,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/355328/?format=api",
    "text_counter": 382,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "The Member for Bura Constituency",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": " Mhe. Spika, nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu. Nakushukuru wewe pia. Natoa kongole kwako na kwa naibu wako. Lakini kwa vile uko hapo leo, wacha niseme kongole kwako kwanza. Mhe.Spika, nachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Koinange kwa kufikiria na kulete Hoja kama hii. Lakini mimi nina tatizo na Hoja hii vile ilivyoandikwa. Ni muhimu kuanzisha matibabu ya dharura kwa Wakenya, hasa wale wanaotoka katika sehemu kame katika nchi hii. Lakini matibabu ya dharura yanaambatana na vitu viwili. Moja ni uchukuzi. Kuna uchukuzi wa ubinafsi na uchukuzi wa umma. Uchukuzi wa umma unaopatikana katika matibabu ya dharura ni ambulensi zinazotolewa naSerikali. Hizo ambulensi hupati bure. Mpaka uzilipie.Utaangalia uchukuzi wa umma na uchukue teksi. Kwa sababu ni haki ya kikatiba, tutasema “Beba mgonjwa hapa, upeleke hospitali bure kwa sababu ni haki ya kikatiba?” Hayo yanawezekana? Hayawezekani. Haki ya kikatiba siyo tukio la siku moja. Haki ya Katiba ni mchakato. Ni lazima tupige hatua manake kuna haki nyingi katika Katiba yetu.Hatuwezi kuamka kesho asuhuhi na sote tupige laini tuseme: “Twataka haki zetu!” Haiwezekani. Sisi kama viongozi ni lazima tuwaeleze Wakenya ukweli. Yale yanayowezekana yatekelezwe kwa mipangilio. Hoja hii inakosa nini, Mhe.Spika? Miaka 50 ya Uhuru, nikizungumzia sehemu ninayowakilisha Bungeni ya Bura, ambayo ina eneo la kilomita 16000 mraba, kuna hospitali moja tu.Ukienda kwa hiyo hospitali, utapata dawa aina tatu kila siku, nazo ni panadol, asprin na ORS. Hauwezi ukayapata madawa mengine. Tuliunda CDF na tukajenga zaidi ya hospitali kumi. Wacha hata dawa, kupata daktari hata leo ni ndoto. Zimebaki tupu na zinaishi popo. Sasa tutakapokuja na fikra zakusema tutoe huduma za dharura bure, ikiwa tumeshindwa kwanza na zile hospitali ziko, je, tunazungumza ukweli? Utekelezaji wake uko? Ningemuomba aliyeileta Hoja hii- --"
}