GET /api/v0.1/hansard/entries/355330/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 355330,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/355330/?format=api",
"text_counter": 384,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "The Member for Bura Constituency",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Mhe.Spika, hiki kidude nikama kimeletwa kutoka Korea. Mtu mrefu kama mimi ni lazima ainame sana. Sijui warefu kama mimi tutapata fursa vipi tupate vyombo ambavyo vitatoa sauti yetu bila kuinama. Nikirudi kwa Hoja, kinachokosekana ni bima ya kitaifa. Bima ambayo kila Mkenya, popote alipo, akiwa mashambani au mji mkuu ataipata. Serikali itakapotoa bima hiyo, itatoa kwa uchukuzi na matibabu. Lakini hivi hivi, hoja hii haiwezi ikatekelezwa. Ndiyo ni ya kimsingi na ni ya haki ya kikatiba, lakini haki hiyo haina mbinu ya vile tutaitekeleza. Kwa hayo machache, nasikitika kuipinga. Ahsante."
}