GET /api/v0.1/hansard/entries/355792/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 355792,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/355792/?format=api",
"text_counter": 429,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1179,
"legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
"slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
},
"content": "Ahsante sana, mhe. Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii. Naunga mkono hoja hii inayohusu masuala ya usalama. Ni jambo la huzuni kuona mambo yaliyofanyika huko Bungoma. Vile vile, ni jambo la aibu kuona kwamba sisi Wakenya tunauana wenyewe. Haifai hata kidogo. Inatupasa kuangalia hili jambo kwa njia nyingi. Tusilaumiane. Sisi kama Wabunge sharti tuangalie jambo hili kwa makini. Rais alisema kwamba atahakikisha kwamba kuna askari mmoja kwa raia 450. Nisingesema tunamlaumu Rais wetu kwa sababu kuna mpangilio wa mambo. Ukisema utaoa si kwamba utamaliza kufanya mambo yote. Huwa kuna utaratibu. Kusema kwamba askari wataajiriwa, lazima pawepo na bajeti ambayo italetwa hapa. Tunaingojea kwa hamu sana ili tupitishe jambo hilo la fedha ndiposa tutimize lengo la Rais wetu. Hata kama tunalaumu Serikali, sisi Wabunge tunalo jukumu kubwa sana kuhusu usalama wa maeneo bunge yetu. Katika eneo langu la Bahati, pakitokea jambo sharti niwe mstari wa mbele kuita Mkuu wa Wilaya na maafisa wakuu wa usalama. Tunao huo uwezo."
}