GET /api/v0.1/hansard/entries/355795/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 355795,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/355795/?format=api",
    "text_counter": 432,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "May 2, 2013 PARLIAMENTARY DEBATES 45 Hon. Ngunjiri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, nimemsikia mwenzangu. Tumechunguza mambo mengi na tunajua. Hata mambo ya wizi wa ng’ombe yanachangiwa na watu waliomo Serikali na Bungeni. Ndiyo maana nikasema tuna jukumu sisi wenyewe. Hatuwezi kuachia suala la usalama maafisa wa usalama tu. Lazima tushirikiane sote. Kama ni Bungoma, rafiki yangu mhe. Wamunyinyi--- Nakushukuru kwa kuzua jambo hili kwa sababu linahusu kila sehemu ya nchi. Hata hivyo, Wabunge wa eneo hilo wana haki ya kuangalia hili jambo kindani. Hawa watu ni watoto wetu. Wengi wao hawajatoka nje. Tunaelewa kwamba tulitaka kuwa na Inspector-General. Tumpatie nafasi aweze kujipanga.Vile vile, tuipatie Serikali ya Uhuru nafasi. Sisi Wabunge lazima tulaani hivi visa vya mauaji vilivyo huko Bungoma. Mhe. Naibu Spika wa Muda, sisemi eti tujipatie kazi nyingine ya usalama, lakini tuhusishwe kama Wabunge! Tuna haki ya kuangalia na kujua ni kitu gani kinasababisha makosa. Ni haki yetu kuangalia hata maji. Tunaweza kusaidia sana kwa kuchangia kutatua shida zilizoko mashinani kuhusu usalama. Kwa hivyo, ni muhimu sana kufanya hivyo kuliko kutoa lawama; kupiga domo. Tuangalie ni njia gani nzuri ya kufanya hivyo ili tuweze kusaidia Serikali. Asante sana."
}