GET /api/v0.1/hansard/entries/355838/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 355838,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/355838/?format=api",
"text_counter": 475,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuunga mkono Hoja hii kuhusu ukosefu wa usalama. Si watu wa Kaunti ya Bungoma ambao wanaathiriwa na ukosefu wa usalama bali ni sisi sote. Nilikuwa ninachangia mambo ya Peace Caravan katika eneo letu. Ningependa kuwapa pole watu wa Kaunti ya Bungoma. Sisi zote tumepitia mambo haya na inafaa tushirikiane ili wauwaji waweze kupatikana haraka. Pia, inafaa viongozi wote wa mashinani washirikiane ili maafisa wa Serikali waweze kujua ukweli kwa sababu maafisa hawajui waelekee wapi. Sisi watu tunaotoka Baragoi, tumeathiriwa kutokana na ukosefu wa usalama tangu 2009. Watu 40 waliuwawa na kukatwa shingo tarehe 17 mwezi uliopita. Tumegundua kwamba ni wale watu tunakaa nao ndio wanachangia vita hivi. Ukiangalia utaona kwamba Tana River, Garissa, Turkana, Samburu---"
}