GET /api/v0.1/hansard/entries/355886/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 355886,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/355886/?format=api",
"text_counter": 32,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
"speaker_title": "The Member for Matuga",
"speaker": {
"id": 2308,
"legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
"slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Spika. Nilikuwa nimevunjika moyo nikifikiria labda Mhe. Spika anafikiria mimi ni marembo ya Bunge hili kwa sababu kila nikiinuka, nanoa. Kwa hivyo, ninakushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii kuzungumza machache kuhusu Marehemu Mutula Kilonzo. Mutula hawezi kusahaulika kwa sababu ya shughuli ambazo alikuwa akifanya. Mimi binafsi, ningetaka kupeleka rambirambi zangu kwa sehemu yake ya uwakilishi Bungeni na pia kwa familia yake. Mhe. Mutula alikuwa rafiki yangu na hata aliwahi kuwa wakili wangu nilipokuwa nimedhulumiwa katika uchaguzi kule Matuga. Ni matumaini yangu kwamba watu watakuwa wastahimilivu na wanyenyekevu kwa sababu Mungu amesema wazi wazi katika Koran na Bibilia kwamba vyovyote vilivyo, siku moja mtu atakufa. Mara nyingi, sisi wanadamu, hasa mtu anapokufa, tunasahau kabisa kwamba amri ya Mungu inasema hivyo. Ni matumaini yangu kwamba familia yake, marafiki zake na watu waliofanya kazi naye, watamuombea ili aweze kuenda mahali pema peponi. Lakini mbali na hayo, ninaunga mkono kwamba Serikali ihakikishe kwamba imejitoa wazi wazi na wale waliowekwa kuchunguza watatoa ushahidi wa"
}