GET /api/v0.1/hansard/entries/355889/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 355889,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/355889/?format=api",
    "text_counter": 35,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kisawasawa na wayalete maneno vile yalivyo. Mara kwa mara tume zimeundwa, lakini tume hizi zote, huangukia pa tupu. Ni matumaini yangu kwamba kutokana na hali hiyo, Serikali tuliyonayo, kulingana na Katiba, itatoa maneno vile yalivyo ili kuondoa wasiwasi kwa kila mtu na kuleta watu wote pamoja. Mambo kama haya mara nyingi hugawanya watu lakini ninawaomba watu wasigawanywe na mambo kama haya kwani kwa vyovyote vile, hata angaliishi miaka mingine zaidi ya mia, bado siku moja Mutula angekufa. Ninawaomba wote walio hapa tusigawanyishwe na kifo cha Marehemu Mutula. Kazi yetu kubwa hivi sasa ni kuhakikisha kwamba sote tunamuombea Mungu kama ndugu na tusiwe watu wa kuenda hivi na vile kwa sababu huyu alikuwa huku na yule alikuwa kule. Hili ni jambo ambalo ni lazima tuliondoe katika fikira zetu. Sana sana, sisi waheshimiwa, tukiwa mahali pamoja bila kujali vyama wala chochote, wale ambao tunawaongoza kule nyumbani, bila shaka, watafuata nyayo zetu kwa sababu Serikali hii iko chini ya Wabunge. Wao ndio wanatengeneza sheria. Kwa hivyo, tukiwa kitu kimoja kama Wabunge na tukiamua kupendana bila kujali misingi ya dini wala ya vyama, nina imani kwamba Serikali hii itakuwa safi na tutaishi vizuri kama watoto wa baba na mama mmoja. Kwa hayo machache, ninaomba familia ya Mutula iwe stahimilivu na sisi marafiki tungojee vile hali itakavyokuwa."
}