GET /api/v0.1/hansard/entries/356860/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 356860,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/356860/?format=api",
"text_counter": 282,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kwa marekebisho hayo yafana na hivi sasa si wakati wa watu kuanza kubishana wakisema kwamba Jubilee inaweza kufanya hivi ama haiwezi. Hii ndiyo hali halisi Wakenya walioitaka. Walipitisha Katiba kwa kuamini ya kwamba kutakuwa na serikali za county. Ukweli ni kwamba ramani ilichorwa na kontrakta kupatiwa kazi. Tukianza kusema kwamba tutamnyima kontrakta vifaa vya ujenzi, hivyo tumpe saruji kidogo aweke mchanga mwingi, jengo lile halitakuwa la maana na mwishowe litavunjika. Kwa hivyo, ninasema hizi serikali za majimbo tuhakikishe tumeweza kuzipa nguvu kwa kuzipa pesa za kutosha kufanya kazi nzuri. Kwa hivyo, ni lazima kuwe na pesa kiasi kwamba nikizungumzia Lamu Mashariki, pesa zilizokuwa zimetolewa hata hazifiki Kshs.1.3 billion na bajeti yao ilikuwa ni Kshs1.8 billion. Kwa hivyo, kwa marekebisho hayo, angalu itafika kama Kshs.1.7 billion. Kwa hivyo, tuhakikishe kwamba zile pesa tutaweza kupeleka kwa counties zitakuwa pesa ambazo zitaweza kufanya kazi kisawasawa and wao waweze kuonekana wameweza kujimudu. Asante."
}