GET /api/v0.1/hansard/entries/357454/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 357454,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/357454/?format=api",
"text_counter": 67,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr). Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Spika. Na mimi pia nasimama kuunga mkono wenzangu na kukubaliana kuwa kuna umuhumu wa sisi kijadiliana kuhusu sheria hii ambayo tunaenda kupitisha ya ugawaji wa pesa kulingana na Katiba ambayo ilipitishwa 2010. Katiba hii imetupatia nafasi ya kuwa na serikali za ugatuzi na vile vile serikali ya juu. Bila shaka Wakenya sasa hivi watakuwa na hali ya wasiwasi na hali ya kuhangaika mpaka tuzoee kuwa kuna serikali za aina mbili; serikali ya kitaifa na serikali ya ugatizi ambayo iko mashinani. Kitu ambacho kinanifurahisha zaidi ni kuwa pia katika maeneo yale ambayo yamebaki nyuma, yaliyo duni kimaendeleo, kuna pesa ambazo ni za kusawazisha hazina ambayo imewekwa ya kuweza kusawazisha maeneo yale kimaendeleo ili tuweze kukimbizana na maeneo yale ambayo yako mbele kimaendeleo. Kwa sasa hivi, pesa ambazo watu walikuwa wamezitarajia, ni nyingi lakini yote hayo ni kwa sababu hakuna mtu anayefikiria kuwa hesabu itakayotumika itakuwa ya mwaka gani. Tuko mwaka wa 2012/2013 na zile pesa zinazotumika ni zile zilikuwa zimetafutwa Serikalini mwaka wa 2011/2012. Wote wanaangalia kuona vile tutaanza shughuli hizi. Ninakubaliana na wenzangu kwamba tukianza shughuli hizi za kuhakikisha kwamba ugawaji wa pesa unatekelezwa sawa sawa kutakuwa na migongano na malalamishi kati ya tume ambayo inasimamia ugavi wa pesa, Serikali ya Kitaifa na serikali za ugatuzi."
}