GET /api/v0.1/hansard/entries/357459/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 357459,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/357459/?format=api",
"text_counter": 72,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr). Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Sisi ambao tuko katika upande wa Serikali tungependelea kufanya kazi na wenzetu ambao wako katika upande mwingine. Sisi wote ni Wabunge. Wale walio wengi na wale walio wachache ni wanachama wa Bunge hili la Kumi na Moja. Kuna umuhimu wa sisi kufanya kazi pamoja. Tumechelewa sasa hivi kwa sababu Kamati ambayo ingeangalia masuala haya bado haijaundwa. Ningependa kuwaomba wenzangu tuungane ili tuangalie masuala haya yanayohusu shughuli hizi ambazo zitawezesha si tu Serikali ya Kitaifa bali serikali za ugatuzi kutekeleza majukumu yao bila shida yoyote. Mwanzo huwa mgumu lakini watu wakifanya kazi pamoja inakuwa rahisi. Hii ni kwa sababu hili ni jambo geni. Ni hivi majuzi magavana, Wabunge na wawakilishi wa kauti walichaguliwa kwa mara ya kwanza katika nchi yetu. Hili si jambo la kawaida."
}