GET /api/v0.1/hansard/entries/357544/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 357544,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/357544/?format=api",
    "text_counter": 157,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Ahsante sana Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono huu Mswada japo kwa shingo upande. Tunazungumzia majimbo kuendelea. Majimbo ni mtoto tuliyemzaa hivi karibuni. Ukimlea mtoto vyema, atakuwa na afya nzuri. Kwa hivyo, ni muhimu na lazima serikali za majimbo zipate mgao ambao unastahili kuendesha miradi. Upande mmoja wa Jimbo la Kwale lina ukame. Upande huo mwingine unaweza kujimudu kidogo. Hakuna maji ya kutosha. Hakuna barabara. Tuna barabara moja tu inayosimamiwa na Serikali; nayo ni barabara ya Kinango-Kwale. Mama anapopatikana na uchungu ndiposa umfikishe hospitalini Kinango, sharti utumie wheelbarrow kilomita zaidi ya 40. Ikiwa hatutapata pesa za kutosha, basi hizo barabara hazitapatikana. Maji yanatoka kwetu lakini hatuwezi kuyanywa. Maji hayo yanapelekwa Mombasa. Gavana asipokuwa na pesa za kutosha, yale maji hatutayanywa. Hilo limechangia maradhi tofauti tofauti yanayotoakana na maji machafu. Imeibuka kuwa sisi tunakunywa maji pamoja na wanyama. Wakati huu wa mvua, hata yale machache ambayo yalikuwa safi huchafuka. Gavana asipokuwa na pesa za kutosha, tutajimudu vipi kimaisha? Viwanda vya Kwale vingi vilifungwa kwa sababu ya ufisadi. Gavana anahitajika kufufua hivyo viwanda na pia kuanzisha viwanda vingine vidogo vidogo. Bila pesa, hataweza kufanya hayo. Hii imechangia ukosefu wa kazi na ndiyo maana hata hali ya usalama hatuna kwetu. Hii bajeti ambayo tunaizungumzia kwa sasa ina uonevu mkubwa sana. Sisi watu wa Pwani tulilia majimbo na tukayapata. Lakini kama hatutapata pesa ambazo zilikadiriwa na Bunge la Kumi, ni kumaanisha tuko katika hali ya kuua majimbo. Magavana lazima wapewe pesa za kutosha; siyo hizi zilizotajwa hapa. Serikali za majimbo haziangalii tu mambo ya barabara. Tunahitaji mambo mengi kujimudu kimaisha hasa sisi akina mama. Sisi hatuna vyeti vya ardhi. Hatuna raslimali zozote zile. Tunahitaji pesa ili tuweze kuanzisha biashara ndogo ndogo. Lazima"
}