GET /api/v0.1/hansard/entries/357547/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 357547,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/357547/?format=api",
    "text_counter": 160,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "tumwezeshe mama apate mikopo nafuu ambayo haina riba kubwa. Je, ikiwa Gavana hana pesa, hao akina mama watajimudu vipi kimaisha? Tunaangazia pia vijana. Sharti vijana watafutiwe njia za kujimudu kimaisha. Wengi wao ni wazazi. Hawana njia za kulea jamii zao. Niyo maana wao huenda kona kutukaba koo na kuchukua mapanga kutukatakata. Serikali za majimbo zinahitaji pesa. Naomba Wabunge wenzangu wachukulie ya kwamba hiki kiwango kilichotolewa na Treasury si kiwango kinachofaa. Sioni kwa nini wamebadilisha. Ama wanataka kuturejesha huko tulikotoka? Walikuwa wanaunda bajeti zao kisha wanatutakaza tuzifuate. Ikizidi, hizo pesa haziteremshwi huko mashinani kwa wakati unaofaa. Wanangojea mwezi mmoja kabla mwaka uishe ndipo wanaleta pesa na ufisadi unaingizwa ndani. Tunaomba Bunge hili likubaliane katika hili jambo. Kama kweli tunataka kutambulika kule mashinani, sharti tuhakikishe kwamba majimbo yamepata pesa. Tuhakikishe kwamba wale Ward Representatives wamepata mishahara inayostahili. Wale ndio macho yetu kule mashinani. Ahsanteni sana. Naunga mkono."
}