GET /api/v0.1/hansard/entries/358154/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 358154,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/358154/?format=api",
    "text_counter": 87,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "May 22, 2013 PARLIAMENTARY DEBATES 11 Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ahsante Mheshimiwa Naibu wa Spika. Nachukuwa fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu na kukushukuru wewe kwa kunipa nafasi hii kujadili mswada huu nyeti. Wanyama, utalii na uchumi lazima viambatane. Ndiposa nchi inawiri ama uchumi wa taifa hili unawiri na Wakenya wafaidike sharti tuwe na sera na mikakati ya kuhifadhi wanyama. Kupoteza ndovu 1,000 katika mwaka mmoja ni hasara kwa taifa letu na vizazi vijavyo. Ikiwa nchi inataka itambulike sharti itunge sheria na sera za kuhakikisha kwamba wanyama hawa hawaangamizwi. Hii ndiyo sababu nimesimama kuunga mkono hii hoja. Huduma ya Wanyama wa Pori (KWS) inayo baraza ambalo limekuwa baraza la kisiasa. Badala ya kubuni sera za maana, kila anapochaguliwa mkurugenzi wa kusimamia huduma hiyo wao hutafuta namna ya kumchimba ili aondolewe ili ufisadi na uuaji wanyama uendelee. Jiulize, ni nani msomi mwenye kiwango chake Dr. Kipng’etich? Ni nini kimechangia kuondolewa kwake? Lazima tuangaze huduma hii tujue inafanya kazi gani. Tusipofanya hivyo wanyama wetu watauliwa kila mara na nchi yetu itapoteza utalii kwa wingi. Ni lazima tuongeze idadi ya askari. Sharti askari wale wapewe silaha na zana za kisasa za kupambana na majangili wanaomaliza wanyama wetu. Lazima askari hao wafunzwe nidhamu vile vile. Ninakotoka kuna Kora National Park. Wapo askari ambao hushika wananchi kiholela kwa sababu moja tu. Badala ya kuwapeleka watu walioshikwa mahakamani Garissa ama Hola ama Mwingi, wao huwazungusha hadi Meru ili wananchi hao wasiitishe msaada. Hii ina maana kuwa ndiyo tuongeze askari, silaha, zana za kisasa na kuwapa nidhamu inawabidi wao askari waache harakati za kisiasa na waende kulinda wanyama. Mheshimiwa Naibu wa Spika, Kipengele 69(e) kinazungumzia kumhusisha mwananchi katika harakati kama hizi. Ikiwa hatutawahusisha wananchi ili kwamba wao wamiliki mbuga hizi kama mali yao ni vigumu kwetu sisi kufaulu katika vita vilivyo mbele yetu. Ingawa mimi ninataka kuunga hoja hii mkono nitatofautiana kidogo na aliyeileta hasa mahali pale pa adhabu. Yeye anapendekeza kwamba kusiwe na bond. Ikiwa katika sheria yetu anayeshukiwa kuwa mwuuaji hupewa bond je, kwa nini tusiangalie haki zao pia? Wapate hukumu kali lakini tusiwanyime bond kwa sababu hiyo ni haki msingi. Hatustahili kuwanyima fursa hiyo. Tuangazie mizozo baina ya wananchi na wanyama. Tutafute suluhisho. Ningependa kutambua jamii ya wafugaji. Asilimia 80 ya mbuga zetu zinapatikana katika maeneo ya wafugaji. Sharti watakaokuja na sera na sheria watambue wafugaji kama sehemu muhimu katika shughuli ya kuhifadhi wanyama. Naunga mkono."
}