GET /api/v0.1/hansard/entries/358173/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 358173,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/358173/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "May 22, 2013 PARLIAMENTARY DEBATES 16 Hon. Simba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Naibu Spika, ningetaka kuongea kwa Kiswahili. Ningetaka kuchangia Hoja hii ambayo imeletwa na Mhe. Ganya. Niko na maoni tofauti kuhusu wawidaji haramu. Katika marekebisho ambayo tunahitaji kuangalia, wawidaji haramu wakipatikana wanafaa kuhukumiwa kifo. Hiyo ni kwa sababu wanafanya nchi yetu isiwe na uwezo na fedha ambazo zinahitajika kusaidia uchumi. Kama si kifo, basi wafungwe maisha gerezani. Kule China, ukipatikana ukijihusisha katika mambo ya madawa ya kulevya, kawaida ni lazima ufe. Kwa uwezo na hekima ya Bunge hili, hii ni sehemu moja ya viegezo vya uchumi wetu. Tunafaa kuhakikisha kwamba jamii ambazo zinaishi na wanyama wa pori zinapewa ridhaa fulani ambayo itawasaidia kama vile mhe. Amina amesema. Hao ndio waliinzi katika mbuga zetu. Mwisho, ningependa kuangazia swala moja. Katika nchi hii, kwa njia moja ama nyingine, tunaabudu watu ambao wamepata fedha kwa njia isiyo halali. Wengi wao ni wawidaji haramu. Pia, wengi wa wawidaji hao wanatumiwa na baadhi ya watu ambao wako na fedha za kutosha. Wengine wako Serikalini na wengine wamepata njia ya kuingia katika mashirika makubwa. Wale wanaopigwa risasi kule msituni huwa wanatumiwa tu. Kama si adhabu ya kifo, wafungwe maisha gerezani. Hivyo ndivyo tutakavyosaidia nchi yetu na kisasi kijacho."
}