GET /api/v0.1/hansard/entries/358178/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 358178,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/358178/?format=api",
"text_counter": 111,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii ili nami nichangie Hoja hii. Namshukuru mhe. Ganya kwa kuleta Hoja hii katika Bunge hili ili tuizungumzie. Mambo ya wanyama wa pori yanafaa tuyazungumzie kwa sababu sisi ndiyo tunaishi nao. Tulizaliwa na kuishi na hao wanyama na tumewachunga kama vile tunawachunga ngâombe na mbuzi wetu. Lakini ajabu ni moja. Wale wanaowachunga na wale wanaoangalia, hakuna faida wanayopata kutokana na wanyama hao. Kuua ndovu ama mnyama yeyote wa pori--- Wenzangu wamepata soko kubwa na ingefaa ijulikane ni ya nani. Sheria ingewekwa ili tujue soko hiyo ni ya nani."
}