GET /api/v0.1/hansard/entries/358179/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 358179,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/358179/?format=api",
"text_counter": 112,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Hiyo ni kwa sababu soko ya meno ya ndovu imewaangamisha watu wengi. Soko hilo linafanya wenyeji wa eneo letu la Samburu, Wamaasai na wafugaji wote kuumia kwa sababu ndovu wanauliwa na kutolewa meno. Wakazi kama sisi hatukuli nyama ya ndovu. Kwa hivyo, unapata ndovu kama 20 wameuawa na wenye wanaowachunga. Hujui wanauliwa namna gani. Kwa hivyo, ningesema kwamba, sisi wengine tunaumia kwa sababu vifaro pia wameisha. Wamebaki kwa wazungu na katika mashamba makubwa. Ukienda katika hifadhi za wanyama wa pori kama vile Hifadhi ya Wanyama ya Samburu, hutapata ndovu. Ukipata, labda mbili au tatu ukibahati. Mhe. Naibu Spika, mashamba ya ranches siku hizi hayafugi ngâombe. Yanahifadhi wanyama wa pori. Ningeomba Serikali ilipishe mashamba hayo kodi kwa sababu ya kuhifadhi wanyama. Wanyama wanapatikana katika mashamba hayo peke yake. Katika biashara hiyo pia, tunasikia kuna mashini ya kusaga meno ya ndovu. Yanabebwa kama unga na kusafirishwa. Kwa hivyo, usalama katika viwanja vya ndege lazima uimalishwe kwa sababu ndovu wamekwisha. Kuna pahali pengine hapa nchini ambako hakuna ndovu. Wamebaki tu katika pande za Wamaasai na Taita. Ni sehemu chache ziko na ndovu na wanyama wengine wa misitu."
}