GET /api/v0.1/hansard/entries/358182/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 358182,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/358182/?format=api",
"text_counter": 115,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Naibu Spika, wanyama wengine kama twiga wameisha kwa sababu wanachinjwa. Hata kuna watu ambao wako na mashini ndani ya mashamba yao. Wanyama wanachinjwa na kuwekwa kwa mikebe. Mwenyewe hajui na kila kitu kinaenda. Kwa hivyo, nashukuru na kuunga mkono Hoja hii. Lazima tutafute njia zozote za kupata pesa ya kuajiri walinzi wa pori ili waweze kulinda wanyama waliopo. Wanyama wa pori wanaisha na tutakuja kulia juu yao. Ningependa kuongeza kwa kusema neno moja; wale watu wanaoishi karibu na wanyama wa pori na wanauliwa na ndovu na wanyama wengine wa pori hawapati malipo. Hakuna malipo na tunapoteza ngâombe na mbuzi kila wakati. Inafaa tuwe na sheria ambayo itahakikisha kwamba wanyama wa pori wakiua binadamu, ni hatua gani itachukuliwa. Tuna shida na tumewapoteza watu wengi. Wakati ndovu anauawa pengine kutokana na hasira kutoka kwa wale ambao wameadhirika kwa kuuliwa kwa watu wao, wale wanaosimamia hifadhi za mbuga za wanyama wanakuja na fujo na kujaribu kupiga watu wote katika manyatta. Lakini, wakati meno ya ndovu yanatolewa na kusafirishwa, hakuna hizo fujo wala ndege kuonekana. Kwa hivyo, nikimalizia, ningependa kusema kwamba lazima hayo yote yaangaliwe kwa sababu tunaumia sana. Nashukuru na naunga mkono Hoja hii."
}