GET /api/v0.1/hansard/entries/358236/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 358236,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/358236/?format=api",
    "text_counter": 169,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon (Ms.) Lay",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1022,
        "legal_name": "Joyce Wanjalah Lay",
        "slug": "joyce-wanjalah-lay"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Naibu Spika wa Muda; ninaamuka kuweza kuchangia Hoja hii. Uwindaji haramu umekuwa kama kidonda sugu hapa nchini Kenya na mahali ambapo mimi ninatoka, ambapo ni Taita Taveta. Tumekuwa na shida nyingi sana kwa sababu ya wanyama. Wakati tunaangalia mikakati ya kuweza kuzuia uwindaji haramu tuangalie pia jinsi gani tunaweza kuwahusisha wananchi katika mambo ya wanyama pori. Vile vile, tunataka wajue kwamba ni jukumu lao kuweza kulinda wanyama pori kwa sababu wataweza kuwaletea faida. Unapata kwamba wananchi wana hasira nyingi sana kwa sababu hawahusishwi katika mambo ya faida kutokana wanyama pori. Hata Jumatatu niliweza kuhudhuria mkutano ambao ulikuwa umewekwa na wananchi pale Mwatate wakiwa na hasira. Wakati mvua imenyesha wanapata mimea, lakini wanakuwa na wasiwasi kwa sababu hawawezi kuvuna hii mimea. Wanyama pori wanakuja kuharibu mimea yao. Akina mama pia wanasema usiku wanashindwa kulala kwa sababu inabidi usiku wavae zile nguo za kujifunika ili kwamba waonekane kwamba pia wao ni vitu vya kutisha wanapotoka nje kwenda kulinda mimea yao. Hilo ni jambo ambalo linahuzunisha sana; wakati tunaangalia hivi inafaa tuweze kusema kwamba wananchi wanaona kwamba hawahusishwi katika mambo ya wanyama pori. Faida ambazo zinapatikana katika mbuga zetu za wanyama pori haziwafikii wale wananchi, na wengi wako katika hali ya umasikini. Wanasema kwamba wana mbuga za wanyama pori na hawapati pesa. Kule kwetu tuna Tsavo Mashariki na Tsavo Magharibi lakini faida yake ni nini? Wanaona kwamba wale wanyama pori wanalindwa zaidi kushinda binadamu."
}