GET /api/v0.1/hansard/entries/358239/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 358239,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/358239/?format=api",
    "text_counter": 172,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hivyo tukiweza kuwahusisha wananchi katika mambo ya kupata faida, na kuwaeleza kwamba wao ambao wako karibu na mipaka ama wanaishi karibu na mbuga za wanyama pori--- Inafaa faida kubwa ipatikane na wananchi ambao wanaishi hapo. Kwa kweli ninajua kwamba wananchi wataweza kuchukua kubuni mbinu na hata mikakati ya kuweza kulinda hawa wanyama pori. Vile vile, utaona kuwa wakiwa na malalamiko, kama vile mwenzangu ametangulia kusema, tuongeze walinzi katika hizi mbuga za wanyama pori. Hawa wananchi ambao wanaishi pale wanahisi kwamba wametengwa. Wakati kazi zinatokea za ulinzi wao hawapatiwi nafasi ya kuajiriwa. Wanasema hata kuna shule za kujifunza hapo lakini vijana wao hawapatiwi nafasi ya kuweza kupata mafunzo ili waweze kupata nafasi za kazi; pia kunao wale ambao wameajiriwa hapo. Wanasema wamekaa kwa miaka mingi na hawawezi hata kupata cheo. Watu wa nje wanapata, ama hupandishwa, vyeo ingawa wao wako katikati ama karibu na hizi mbuga za wanayama pori. Kwa hivyo, wakati ambapo tunaanglia ni mbinu gani ambazo tutaweza kuchukua na kuweza kuzuia uwindaji haramu ni vizuri tuangalie kiini cha uwindaji haramu. Kinaweza kuwa ni umasikini, ama ni wananchi ambao wanaona kama wametengwa. Tujaribu kuwajumuisha. Wakati tunawinda wanyama pori wanatokea katika mipaka yetu. Kama ni katika port wanatokea hapo. Kwa hivyo, ni lazima tuwahamasishe watu ambao wanaangalia pembe hizi zikitoka na hawasemi kitu mpaka zinashikwa katika nchi zingine za nje, na hali sisi hapa Kenya tuna nafasi ya kuweza kuzuia mambo kama hayo. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hivyo, mimi naunga mkono Hoja hii. Asante sana."
}