GET /api/v0.1/hansard/entries/358241/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 358241,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/358241/?format=api",
"text_counter": 174,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Duri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1039,
"legal_name": "Halima Ware Duri",
"slug": "halima-ware-duri"
},
"content": "Asante sana Bw. Naibu Spika wa Muda. Kwa majina mimi ni Halima Ware Duri kutoka Tana River. Mimi ningependa kuchangia Hoja hii. Watu wa KWS ni watu ambao wanalinda wanyama kuliko watu. Nikisema hivyo, kuna mnyama anaitwa nyati. Mnyama huyu anaishi katika Tana River. Hawajaweka ua na hawajazuia wanyama kuingiliana na wananchi ama kuingiliana na mifugo wa nyumbani. Wanyama hawa wanaendelea kuua watu na mifugo. Katika eneo za Wenje, Mnazini, Haroresa na Hara watu wengi wameumizwa na huyu mnyama na hatujaona watu wa KWS wakichukua hatua. Lakini wakati ambapo wanataka kuleta mswada wa pembe za ndovu wanataka tuwasaidie kwa haraka sana. Jambo lingine ambalo ningependa kuongeza ni kwamba kuna mnyama ambaye anaishi ndani ya maji, na ambaye anaitwa âmambaâ ama ângwenaâ. Watu wa Tana River wanachota maji yao kutoka mto Tana, na wakati wanachota maji mnyama huyu hakosi kuua watu zaidi ya watatu kila wiki na hatujaona watu wa KWS wakija na usaidizi wa aina yoyote. Huyo mnyama anaua mifugo ama watu. Kwa hivyo, sisi tunataka watu wa KWS kwanza kabla hatujapitisha Hoja hii ingawa tunaipigia debe, waje waweke ua na wazuia wanyama hao wasiingilie mambo ya wananchi na wasiuwe wananchi ama mifugo yao. Bw Naibu Spika wa Muda, jambo lingine ambalo ningependa kusema ni kuwa lazima KWS walete uhusiano mzuri na wananchi ambao wanaishi na wao. Hapo awali kuna wakati ambapo wakiandikisha wahifadhi walipatia nafasi wale watu ambao ni majirani zao, lakini hivi karibuni hakujakuwa na jambo kama hilo. Wanaandika bila kujali majirani wao, na kama wangetia maanani suala la majirani ambao wanaishi karibu"
}