GET /api/v0.1/hansard/entries/358245/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 358245,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/358245/?format=api",
"text_counter": 178,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Jambo lingine ni kuhusu nyati na vile anavyorandaranda na kuharibu mashamba na maisha ya watu. Huyu ni mnyama hatari sana. Maafisa wa pori wanafaa kwanza kulinda Tana River na kuhakikisha kwamba nyati hali watu wala mifugo, na amezuiliwa ili asiingie kwa mashamba ya watu. Hili ni shirika ambalo lilianzishwa zamani, baada ya sisi kutoka kwa ukoloni. Lina pesa za kutosha na ni lazima wawafundishe wananchi ili wananchi wajue kuwa wanyama wa pori ni muhimu, na kuna umuhimu wa kuwalinda wanyama hao. Kama hawawafunzi watu umuhimu wa wanyama wa pori, watu watawaua wanyama hawa nao wanyama watawaua wananchi. Mwezi wa Disemba wakati wa kampeni, wanaume sita, wengine wao wakiwa wa jamii yangu, waliuawa na wafanyikazi wa porini. Tulipoenda kwa mazishi, tulipata kuwa hao watu walikuwa fukara wa mwisho, na hata kuku hawana. Kwa hivyo, KWS inafaa kuwatia nguvuni watu, na si kuwaua, na kuwashtaki mahakamani. Ingekuwa vizuri kama wangewapatia kazi ya porini kuliko kuwapiga risasi kwa sababu wake zao wakibaki, hawawezi kuendelea mbele. Uwindaji haramu ni mbaya na kupiga watu risasi pia ni haramu kulingana na sheria za Kenya. Kwa hivyo, ni lazima KWS itengeneze namna ya kuwasaidia wananchi na wananchi wanaweza kuwasaidia wanyama. Kuna mnyama anayeitwa fisi, lakini sijui maafisa wa KWS walimweka wapi."
}