GET /api/v0.1/hansard/entries/358302/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 358302,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/358302/?format=api",
    "text_counter": 235,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwamkale",
    "speaker_title": "The Member for Rabai",
    "speaker": {
        "id": 2672,
        "legal_name": "William Kamoti Mwamkale",
        "slug": "william-kamoti-mwamkale"
    },
    "content": " Asante Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Naomba kuchangia kwa kuunga mkono Hoja hii; ni kweli kabisa kwamba utalii unachangia pakubwa uchumi wetu na huleta pesa za kigeni. Nia ya Rais wetu ni kuongeza idadi ya watalii wanaofika hapa kutoka milioni mbili mpaka milioni tatu, lakini tukumbuke kwamba ili kufanya hivi ni lazima tuangalie vile vitu vinavyoleta watalii katika Kenya yetu. Imesemwa hapa kwamba wanyama pori wanachangia pakubwa kuja kwa watalii wengi katika nchi yetu. Kwa hivyo, tuna jukumu kama nchi kuhakikisha kwamba tunachunga wanyama pori wetu."
}