GET /api/v0.1/hansard/entries/358303/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 358303,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/358303/?format=api",
"text_counter": 236,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwamkale",
"speaker_title": "The Member for Rabai",
"speaker": {
"id": 2672,
"legal_name": "William Kamoti Mwamkale",
"slug": "william-kamoti-mwamkale"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, imesemekana kwamba hatuwezi, kama Serikali kuweka mikakati ya kuchunga wanyama pori kama wale wanaoishi na wanyama pori, jamii ambazo zinapakana na mbuga zetu za wanyama pori. Tukitaka kuchunga wanyama pori ni lazima tutambue wale wanaoishi karibu na wanyama hawa. Tuhakikishe kwamba mambo yao ama wao wanawekwa katika mstari wa mbele katika uchungaji wanyama pori. Tumeona katika nchi hii siku za nyuma - siku chache tu zilizopita - jamii zinazoishi karibu na mbuga zetu zilichukua mishale na silaha nyingine na kutaka kuingia msituni na kuwakatakata wanyama pori; hii ni kwa sababu Serikali inaonekana, hasa shirika linalosimamia wanyama pori, kujali wanyama pori zaidi kuwashinda binadamu. Wakati wanyama pori wanapoingilia mimea na kuuwa watu Serikali haionekani kushtuka. Lakini mnyama anapokufa watu wale wanaoishi katika---"
}