GET /api/v0.1/hansard/entries/358316/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 358316,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/358316/?format=api",
"text_counter": 249,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadime",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": "Jana usiku katika maeneo ya Mwakitau, Sorongo na Mwachapo mimea ya watu iliharibiwa sana na wanyama pori. Hatuwezi kusema watu wa Kenya Wildlife Service (KWS) hawana vifaa. Mwezi jana nilikuwa Voi Safari Lodge na nikawa nauliza: Kwa nini Voi Safari Lodge inalindwa na polisi? Niliambiwa wakati walikuwa wanalindwa na watu wa KWS walikuwa wakiibiwa mara kwa mara, na hii ilimaanisha kuna tatizo fulani katika KWS. Mwenye kuleta hii Hoja, Bw. Ganya, nampongeza, lakini yafaa tuijadili kwa upana zaidi. Inahitaji marekebisho mengi sana maanake kuna tatizo kubwa sana."
}