GET /api/v0.1/hansard/entries/358603/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 358603,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/358603/?format=api",
    "text_counter": 268,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Swali la pili, ukisoma Hoja inasema hawa wanatoa mali gafi lakini hawapati faida kabisa. Kama kweli hawapati faida, anavyodai aliyoileta Hoja, ni kwa nini uhamishe upeleka mashinani shida hizi? Mhe. Naibu Spika, jambo la tatu ambalo linanipa matatizo kuelewa ni kuwa, anasema Serikali ya ugatuzi haina uwezo wa kiuchumi kisha anataka tuchukue mashirika ya kiserikali na tuyapeleka kule. Hapa anatuchanganya. Hoja hii haitoi mwongozo na nitaipinga. Miaka ya themanini, Benki ya Dunia ilitoa sera ya Structural Adjustment Programme ambayo imetunyang’anya na kudhalilisha mashirika yote katika nchi hii. Leo, mashirika haya yameanza kufufuka na tunataka kuyapeleka mashinani. Katika Serikali ya ugatuzi, malalamiko ni mengi kama vile maswala ya fedha na sera. Ni vipi tutapeleka mashirika haya? Je, tutakapokosa suluhisho kwa matatizo yanayotukumba, njia rahisi ni kuyasukuma mashinani? Iwapo kuna matatizo ya kiuchumi, tunastahili kutafuta suluhisho kama Serikali kuu. Utajiuliza mada ya Serikali kukuja na mashiriki ya Serikali ni nini. Kila shirika ambalo liko hapa lina lengo, mada na maudhui."
}