GET /api/v0.1/hansard/entries/358606/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 358606,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/358606/?format=api",
"text_counter": 271,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Shirika la Nyayo Tea Zones, lengo lake kubwa sio kilimo wala ni uhifadhi wa mazingira. Swali nyeti ni kuwa: Ikiwa leo utahamisha mashirika ya kilimo kwa kaunti, kesho, mimi nitaleta Hoja, kwa sababu ninatoka Pwani, ya kusema kuwa mashirika ya uchukuzi yakiwemo Bandari la Mombasa na Kenya Ferry yapelekwe kwa kaunti ya Mombasa. Mbunge mwingine ataleta Hoja kusema kuwa kwa sababu petroli imepatikana Turkana, mashirika ya kawi ipelekwe huko Turkana. Lengo la Serikali kuu ni nini? Serikali kuu itapata raslimali ya kuendesha serikali za kaunti wapi? Ni wakati wetu sisi kama Wabunge tufikirie taifa. Kuna tofauti baina ya ugatuzi na majimbo. Huu tunao ni ugatuzi ambao unategemea Serikali kuu. Kwa hivyo, tukatapohamisha mashirika ya Serikali, Serikali itapata raslimali wapi ya kuendesha maswala ya ugatuzi? Kwa hayo machache, ninapinga Hoja hii ambayo ni hatari sana kwa taifa la Kenya."
}