GET /api/v0.1/hansard/entries/358910/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 358910,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/358910/?format=api",
    "text_counter": 195,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kombe",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 250,
        "legal_name": "Harrison Garama Kombe",
        "slug": "harrison-kombe"
    },
    "content": "Nilikuwa nikieleza kwamba maafisa wa usalama wanapofika kwenye maeneo kulikofanywa ugaidi, badala ya kutafuta ukweli wa mambo ili waweze kuwafuata wahalifu vilivyo, wao huwavamia watu wasio na hatia, kama vile wakulima, na hata watoto wa shule. Ninasema hivi nikizingatia kitendo kilichofanyika Malindi wakati Casino ilipovamiwa. Watoto wa shule katika sehemu za mashambani walivamiwa na maafisa wa polisi, wakatandikwa na baadhi yao kukamatwa na kufungiwa korokoroni. Vijana hao waliwekwa korokoroni kwa muda wa siku nane na kuachiliwa bila ya kufunguliwa mashtaka yoyote."
}