GET /api/v0.1/hansard/entries/359708/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 359708,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/359708/?format=api",
"text_counter": 172,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Aburi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2901,
"legal_name": "Lawrence Mpuru Aburi",
"slug": "lawrence-mpuru-aburi"
},
"content": "Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa hii nafasi. Hakuna mtu aliye na taabu zaidi ya mchungaji. Hawa watu hawavai viatu wala nguo nzuri. Juzi tulikuwa na mkutano mkubwa ambao ulihudhuriwa na Wabunge wa Samburu ya Magharibi, Igembe ya Kati, na Igembe ya Kusini. Mkutano huo ulikuwa juu ya mifugo. Wananchi wanateseka sana wakati wa kiangazi kwa sababu mifugo hawapati maji. Kila mtu analia kwamba hakuna maziwa na nyama. Wakati wa kiangazi anayefuga hawa wanyama huzidi kutaabika. Serikali ya Jubilee siyo mbaya; ni Serikali nzuri. Watu wetu wa CORD ni lazima tusikizane nao. Ni lazima tupendane katika Bunge hili ili tuwe kitu kimoja. Katika Kimeru husemekana kwamba atakayeoa mamako ndiye babako. Tuachane na mambo ya Jubilee ama CORD. Tuongee juu ya masuala muhimu hapa. Ule ulikuwa ni mpira uwanjani. Tulicheza na CORD ikaingiza kwa mguu nayo Jubilee ikaingiza kwa mkono ikasemekana kwamba muungano wa CORD---"
}