GET /api/v0.1/hansard/entries/359887/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 359887,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/359887/?format=api",
    "text_counter": 351,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Katika eneo langu la uwakilishi bungeni la Lamu Mashariki, watu hawajui kwamba Serikali inatoa hizi pesa. Asilimia mbili tu ya wazee walioko Lamu Mashariki ndio wamefanya kazi katika mashirika ama Serikali lakini asimilia 98 ni watu ambao wanafanya kazi kwa jua kali; kazi zao za kibinafsi kiasi cha kwamba wakifika umri huu, huwa hawajitambui; hawajui ni nani atakaye wasaidia. Kwa hivyo, naomba na kuunga mkono Hoja hii. Tuhakikishe ya kwamba yale ambayo tutapitisha yatasaidia wazee wetu wafaidike. Tuhakikishe kwamba hawa wazee wetu wanapata usaidizi katika hospitali na kupata pesa ambazo Serikali inatoa kwa wazee kila mwisho wa mwezi."
}