GET /api/v0.1/hansard/entries/360395/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 360395,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/360395/?format=api",
"text_counter": 131,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms) Chidzunga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Nimesimama kuchangia Hoja hii kwa sababu sehemu ninayotoka ni kame. Wanyama wetu wamekufa; wanyama wetu hawafi tu kwa sababu ya mafuriko, bali pia kwa sababu ya njaa na maradhi. Tegemeo langu katika kuunga mkono Hoja hii si tu ili wafugaji wapate bima, lakini naomba Hoja hii ifanyiwe ukarabati ili kuwe na unyunyuziaji maji maeneo kame. Hili likifanyika watu wetu watakuwa na nyasi za kutosha kulisha mifugo yao. Wafugaji wenzetu walio katika sehemu za Kasikazini Mashariki mwa nchi huishia kuja sehemu zetu kwa sababu kwetu nyasi huchukua muda kukauka. Kule kuja kwao huchangia ukosefu wa usalama. Wakati mwingine wakija hata hawaombi ruhusa kulisha mifugo wao huko kwetu. Wao huleta wanyama wao na kuwaingiza katika mashamba ya watu, kisha fujo hutokea."
}