GET /api/v0.1/hansard/entries/360616/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 360616,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/360616/?format=api",
    "text_counter": 352,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bedzimba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1933,
        "legal_name": "Rashid Juma Bedzimba",
        "slug": "rashid-juma-bedzimba"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, ningeomba hii iwe kama mazungumzo yangu ya kwanza katika Bunge. Nilisimama tu kuunga mkono Hoja nilipopata nafasi. Nashukuru Mwenyezi Mungu amekuwezesha kuniona. Nimekuwa nikisimama nikikaa hapa tangu nije. Nikianza na Hoja hii, ninaunga mkono vilivyo kwa sababu wazee si watu wa kutupwa. Wazee wamefanyia mengi taifa hili ambalo linahitaji kuangaliwa kwa uangalifu zaidi. Wazee wa miaka 60 na zaidi, wengi wao hawana ajira. Wengi wao wamestaafu na wengine hawajawahi kuajiriwa kabisa kwa sababu ya kujitegemea wenyewe kwa kazi zao za kibinafsi. Wazee hao wamekuwa mizigo kwa vijana wetu. Imekuwa wazee wanawategemea vijana na ilhali hali ya vijana ni ngumu kimaisha, hata ajira hawana. Hata sasa unakuta vijana wanaanza kukosana na wazee wao. Hata sehemu nyingi wanawaita wazee wao wachawi. Hata inafikia wakati wanaanza kuwaua. Sio kwamba wale wazee wameroga watoto. Wale watoto wanafahamu vyema kwamba hawa wazee wamewalea tangu utotoni, itakuaje hivi sasa wamekuwa wachawi? Kama wangekuwa na malengo mabaya wangeyatimiza wakiwa wachanga. Lakini kwa sababu ya hali ngumu ya maisha, wanaona njia rahisi ya kuondoa mzigo huo ni kusema kwamba hawa wazee ni wachawi. Hii Serikali, ninaweza kusema kwamba imepuuza wazee wetu. Hata mikasa mingi ambayo tunapata katika taifa nzima ni kwa sababu ya wazee. Kwa roho zao hawana raha. Kwa mfano, ukosefu wa usalama katika taifa, mafuriko na mambo mengi mazito yanatokana na kwamba wazee wetu hawana raha na wanaona kama wametengwa. Nikikupa habari, kuna wazee wamekuwa katika nyumba ya muwajiri wao miaka miwili sasa katika hoteli za African Safari Club wakidai malipo yao. Wazee wale walikuja katika Bunge la Kumi hapa, wakazungumza na kamati husika lakini hadi wakati huu shida yao haijasuluhishwa. Wale wazee wana---"
}