GET /api/v0.1/hansard/entries/360623/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 360623,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/360623/?format=api",
    "text_counter": 359,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "viapo. Hatujui lengo lao hasa. Tuko hapa kwa masilahi ya taifa, tuwache tofauti za vyama mbali tuunde kamati husika. Tujadili usalama wa taifa kwa ndani kwa maslahi ya watu wetu wa taifa hili. Nikimalizia, ningekuomba katika matamshi yetu kama viongozi tuwe makini sana. Wananchi wa Kenya wanatuona katika runinga na kutusikiza. Huenda tukawagawanya Wakenya kwa sababu ya matamshi yetu. Ningekuomba, kama Mbunge yeyote atasimama kuzungumzia jambo la ukabila, dini au dhehebu lolote, uwe unamsimamisha kwa sababu wananchi wanamsikiza kwa makini na huenda matamshi hayo yakaleta tofauti kubwa katika taifa letu. La mwisho ni kwamba ningeomba tatizo la ardhi liangaliwe kwa makini sana na hiki ndicho chanzo cha kila kitu. Ikiwa tutaweza kutatua matatizo ya ardhi, basi taifa hili litakuwa na amani zaidi. Ningeomba hili Bunge la Kumi na Moja lipitishe sheria ambayo itawasaidia kupunguza shida ya maskwota na kuwalinda mwananchi wa Kenya dhidi ya dhuluma ya wale wanajiita wenye mashamba. Asante sana!"
}