GET /api/v0.1/hansard/entries/361133/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 361133,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/361133/?format=api",
    "text_counter": 501,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Bi. Naibu wa Spika, hii ni heshima kubwa kwa taasisi ya Bunge na Wabunge. Mawazo ni tofauti. Baadhi yetu wanasema kwamba asilimia fulani ya Mawaziri wateule wanatoka mkoa fulani na asilimia fulani wanatoka mkoa mwingine. Lengo na maudhui ya kubuni Serikali ni kuhudumia wananchi. Inafaa wale wanaoleta hoja hii wakumbuke kwamba Serikali iliyopita ilikuwa ya sehemu mbili za nchi hii. Zaidi ya asilimia 50 ya Mawaziri wa Chama cha ODM walitoka Mkoa wa Nyanza. Kwa nini wakati huo wenzetu hawakushangaa? Mbona leo wanaona ajabu?"
}