GET /api/v0.1/hansard/entries/361160/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 361160,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/361160/?format=api",
    "text_counter": 528,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Bi. Naibu wa Spika, nikiendelea, lengo na maudhui yetu ya kuangalia uteuzi wa Mawaziri hivi leo ni kutoa huduma kwa nchi ya Kenya. Nimetoka katika sehemu ya Tana River. Tunavyozungumza, barabara zimekatika katika sehemu hiyo. Zaidi ya watu 10,000 hawana makao. Je, tutamkimbilia nani kwenye ofisi ya Wizara husika kuomba usaidizi ili wakazi wa sehemu hiyo wapate huduma? Mizozo imeibuka kwenye kila pembe ya nchi hii. Ni vipi tutapata Waziri haraka atoe huduma inayostahili ili tupunguze ukabila na siasa za vyama? Tunataka tupate Mawaziri ili watoe huduma kwa Wakenya kwa sababu wao hawatakwenda kuuliza ni nani anayetoka Nyanza ama Pwani. Watatoa huduma kwa Wakenya wote, kama Mawaziri wa Serikali. Tumeelezwa mengi na Wanakamati wa Kamati ya Uteuzi kuhusu Bi. Kandie. Lakini Wanakamati hao hawakutuambia iwapo mteule huyo hana elimu ya kutosha ama ni mfisadi ama ana matatizo ya kiutu ama ya kitaaluma. Kamati hiyo imetuambia kwamba Bi. Kandie hafai. Je, imekuwaje hafai? Niliisoma Katiba, na haswa Kifungu husika – Kifungu 12(a) na (b). Hadhi ya Kamati ya Bunge ya Uteuzi ni sawa na ile ya Mahakama Kuu. Kamati ya Uteuzi ina uwezo wa kumshurutisha mtu yoyote kuleta habari yoyote inayohitajika kwa shughuli ya Kamati hiyo. Unapokosa kuitumia fursa hiyo na kuleta Bungeni Ripoti ambayo haiambatani na maono yako na kutuambia kwamba Bi. Kandie hafai kuhudumu kama Waziri, unatuambia nini? Wakenya wanaliangalia Bunge hili. Si kila mtu ambaye atapata fursa ya kusimama hapa na kuzungumza jinsi ninavyozungumza. Ukipewa wajibu wa kutunga sheria na kuamua ni nani anayefaa kuwa Waziri, ni lazima utekeleze wajibu huo kwa haki na uadilifu. Tusizingatie maumbile ya kijinsia ya mtu huyo ama sehemu anakotoka."
}