GET /api/v0.1/hansard/entries/361291/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 361291,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/361291/?format=api",
    "text_counter": 659,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi Country Women Representative",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 691,
        "legal_name": "Aisha Jumwa Katana",
        "slug": "aisha-jumwa-katana"
    },
    "content": "(Hon. (Ms.) Katana): Mhe. Naibu Spika, mimi ni mheshimiwa Aisha kutoka Kilifi. Kwa vile ni mara yangu ya kwanza, naomba uniruhusu niwapongeze watu wa Kilifi kwa kunichagua ili niwaakilishe katika Bunge hili la Kumi na Moja. Nimesimama kuunga mkono orodha ya majina. Nimeipitia Ripoti hii kwa uchache na nikaona kwamba walioteuliwa wana tajriba na taaluma ya kutosha kuendesha Wizara walizotengewa. Kuhusu suala la ukabila, nafikiri Katiba imeangazia hilo jambo katika Kipengele cha 152 (d); kwamba si chini ya Mawaziri 14 na si zaidi ya 22. Katika taifa letu, tuna makabila 42. Wenzangu waliozungumza awali wametaja kwamba kuna ugumu fulani unaojitokeza. Hata ikiwa Rais angeamua kuwepo na Wizara 22, bado haingeweza kufikia idadi ya makabila tuliyonayo katika taifa hili. Mimi naona kwamba hakuwachagua kwa kuzingatia kabila ila ametumia misingi ya elimu na tajriba waliyonayo ili watumikie Wakenya wala siyo makabila yao. Mimi naamini kwamba wanao uwezo---"
}