GET /api/v0.1/hansard/entries/361604/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 361604,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/361604/?format=api",
"text_counter": 262,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nakara",
"speaker_title": "The Member for Turkana Central",
"speaker": {
"id": 2926,
"legal_name": "John Lodepe Nakara",
"slug": "john-lodepe-nakara"
},
"content": " Mhe Spika, asante sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hoja ya Mhe John Ngâongo. Pia nataka kuchukua nafasi hii kutoa hotuba yangu ya kwanza; katika siku za nyuma sikupata nafasi kamili ya kupeana hotuba yangu ya kwanza Bungeni. Ninaitwa Mishonari Lodepe Nakara, Mbunge wa Turkana ya Kati. Ningependa kuchukua nafasi hii kushukuru watu wa Turkana ya Kati kwa kunichagua na kunifanya kuwa Mbunge wao wa kwanza chini ya Katiba mpya.Turkana ya Kati ni moja ya maeneo ya Bunge ambayo yako katika kaunti ya Turkana, na ni moja ya maeneo ya Bunge ambayo yamekuwako tangu Kenya ipate Uhuru; nawashukuru wananchi wa Turkana ya Kati kwa kunichagua kuwawakilisha katika Bunge hili la Kumi na Moja."
}