GET /api/v0.1/hansard/entries/361605/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 361605,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/361605/?format=api",
"text_counter": 263,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nakara",
"speaker_title": "The Member for Turkana Central",
"speaker": {
"id": 2926,
"legal_name": "John Lodepe Nakara",
"slug": "john-lodepe-nakara"
},
"content": "Nikichangia Hoja ambayo iko mbele yetu, ningependa kusema kwamba kama kuna wavuvi ambao wanaumia, ama wanateseka sana katika nchi ya Kenya, ni wavuvi wa Ziwa Turkana; shida yao ni mambo yafuatayo, kwanza ni barabara. Barabara inayoelekea Ziwa la Turkana, ambalo kubwa katika nchi hii, ni barabara ambayo ni kama inayoenda mbinguni. Ina shida nyingi. Magari yanaharibika. Kuna mashimo mengi barabarani. Usalama ni mbaya na umefanya wavuvi wasiweze kupeleka mazao yao katika miji iliyo karibu na Ziwa la Turkana ili kupata soko. Hilo ni tatizo moja ambalo wavuvi wa Turkana wanapata."
}