GET /api/v0.1/hansard/entries/361606/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 361606,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/361606/?format=api",
    "text_counter": 264,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nakara",
    "speaker_title": "The Member for Turkana Central",
    "speaker": {
        "id": 2926,
        "legal_name": "John Lodepe Nakara",
        "slug": "john-lodepe-nakara"
    },
    "content": "Bw. Spika, tatizo la pili ni soko. Nilishangaa juzi nilipoenda kwenye hoteli moja hapa Nairobi, na kuagiza nipewe samaki. Samaki niliyoletewa kule kwetu Turkana inauzwa Kshs20. Hapa niliuziwa Kshs200. Nilishangaa sana. Nilisema kama tungekuwa na soko kama hiyo samaki ambao tunauza Kshs20 huko Turkana hata tukiiuza Kshs50 itakuwa ni faida kwa watu wa Turkana. Naiomba Serikali iangalie jinsi ambavyo wavuvi wa Turkana wanaweza kuleta samaki katika mji wa Nairobi ili wapate soko nzuri."
}