GET /api/v0.1/hansard/entries/362113/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 362113,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362113/?format=api",
"text_counter": 309,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Masikitiko makubwa ni kwamba sekta ya uvuvi katika eneo la Pwani imedharauliwa sana na Serikali kwa sababu tunazoshindwa kuzielewa. Hivi sasa, ukienda kuulizia katika afisi za uvuvi, utapata kwamba licha ya kwamba Pwani ni eneo kubwa sana la uvuvi kwa sababu ya Bahari Hindi, kiasi cha samaki wanaopatikana ni kidogo sana ukilinganisha na kiasi cha samaki wanaopatikana katika Ziwa Victoria na kwingineko. Kusema kweli, hili ni jambo la kushangaza sana. Tukiangazia zaidi, watu wanaofanya kazi hii katika maeneo ya Lamu na kwengineko, na haswa tukiangazia suala la vifaa vya kuhifadhia samaki, kama lilivyozungumziwa; huwezi kuvipata vifaa hivyo katika sehemu hiyo. Vifaa hivyo vikiweko, vitawasaidia wavuvi kuendeleza kazi hiyo kwa njia bora zaidi."
}