GET /api/v0.1/hansard/entries/362114/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 362114,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362114/?format=api",
    "text_counter": 310,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika, maskitiko makubwa ni kwamba tatizo kubwa linaloikabili jamii ya wavuvi katika maeneo ya Lamu na sehemu nyingine za Pwani ni kwamba, jamii hiyo haijawahi kusaidiwa ili iweze kujiendeleza. Utapata watu kutoka nchi zingine kama vile Indonesia na China wanakuja kuvua samaki katika maeneo ya nchi yetu kwa sababu wako na vifaa vya kisasa, yakiwemo maboti mazuri yanayowawezesha kufanya kazi hiyo kwa njia bora zaidi. Wanakuja kuvua samaki katika sehemu ya nchi yetu na kuwapeleka samaki hao kwao kwa faida ya nchi zao na faida zao binafsi. Chombo kinachotumiwa na watu wetu kwa shughuli ya uvuvi hakiwezi kumudu na kuwawezesha wavuvi wafaidike."
}