GET /api/v0.1/hansard/entries/362118/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 362118,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362118/?format=api",
"text_counter": 314,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ndani ya mtaa. Hakuna sehemu maalumu iliyotengwa na Serikali kwa wavuvi kuuzia samaki wao. Utaona kwamba mazao ya samaki yanayotoka katika sehemu za Lamu yanapelekwa kuuzwa kiholela, kama kwamba sekta hii haina maana na mwelekeo katika nchi yetu. Mhe. Naibu wa Spika, kutokana na madharau hayo, ama kutokana na kutozingatiwa kwa suala hili; huweza kupata mvuvi hata mmoja ambaye ana mwelekeo mzuri maishani. Wavuvi wameshindwa kuwaelimisha watoto wao na kujiendeleza kimaisha kwa sababu ya hali hii ambayo tunaizungumzia. Naamini ya kwamba kama Serikali ingekuwa na mikakati maalumu ya kuwasaidia wavuvi, wao pia wangenawiri na kuweza kujiendeleza kimaisha kama Wakenya wengine wanavyojiendeleza."
}