GET /api/v0.1/hansard/entries/362122/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 362122,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/362122/?format=api",
    "text_counter": 318,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Hivi sasa, Lamu kunajengwa bandari. Hata ikiwa ujenzi huo utakamilika miaka mitano ama kumi inayokuja, napendekeza kutengwe sehemu maalum kwenye bandari hiyo, ambako wavuvi watakuwa wakiwapeleka samaki wao na kuweza kuwasafirisha hadi mahali popote watakapotaka bila ya kuhangaishwa ama kuwa katika hali ya sitofahamu kutokana na kutojua mahali pa kuwapeleka samaki wao. Kwa hivyo, ni lazima kuwe na sehemu maalumu katika bandari inayojengwa, ambako wavuvi watakuwa wakiwahifadhi samaki wao."
}